IKIWATEGEMEA washambuliaji wake wa kimataifa, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wanaocheza TP Mazembe ya DR Congo, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo jioni inakabiliana na timu ya taifa ya Malawi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya FIFA.
Mechi hiyo inayotarajiwa kurushwa moja kwa moja 'Live' na Azam TWO ya Azam TV inapigwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kuanzia majira ya saa 10:00.
Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Baraka Kizuguto ameuleza mtandao huu asubuhi hii kuwa wachezaji wote wa Stars wako salama.
"Tunamshukuru Mungu vijana wote wameamka salama, ni jukumu la kocha Mart (Nooij) kupanda nani aanze. Morali ni kubwa na tunatarajia ushindi ili kupanda viwango vya FIFA". Amesema Kizuguto.
0 comments:
Post a Comment