Wes Brown na John O'Shea walijaribu kumzuia Radamel Falcao ndani ya boksi la penalti
KOCHA wa Sunderland, Gus Poyet usiku wa jana hakuridhishwa na maamuzi ya refa ya kumuonesha kadi nyekundu Wes Brown, timu yake ikilala 2-0 dhidi ya Manchester United uwanja wa Old Trafford.
Mwamuzi wa mechi hiyo Roger East alimuonesha kadi mchezaji ambaye sio sahihi, hivyo Poyet anataka teknolojia ya kuwasaidia waamuzi lazima itafutwe.
Sunderland walikaza mpaka dakika ya 63 lilipotokea tukio la Jon O'Shea kumuangusha Radamel Falcao katika eneo la penalti, wakati huo Wes Brown alifika eneo la tukio baada ya sekundu chache
Ingawa ilikuwa penalti ya wazi, East amlitia 'umeme' yaani kadi nyekundu Brown akidai alimfanyia madhambi Falcao na hali hii imemfanya Poyet afungue mdomo wake akieleza namna alivyokerwa na maamuzi hayo.

Manchester United walipewa penalti, lakini Brown alipewa nyekundu badala ya O'Shea

Roger East amesisitiza kuwa kulikuwa na faulo mbili, moja ilifanywa na Brown aliyepewa kadi nyekundu.
"Mwamuzi aliwaambia wachezaji kulikuwa na faulo mbili, moja ilifanya na O'Shea na nyingine na Wes Brown. Aliadhibu ya Wes Brown na kumpa kadi nyekundu. Wes Brown hakumgusa mtu yeyote, sijui aliona kitu gani". Amesema Poyet.
0 comments:
Post a Comment