Klabu ya Sunderland imemtimua kocha wake Gus Poyet baada ya uongozi wa timu hiyo kutoridhishwa na kiwango cha kikosi hicho tangu msimu huu uanze.
Poyet ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea alianza kuwafudisha paka hao weusi Oktoba 2013 akichukua mikoba ya muitalia Paolo Di Canio na kufanikiwa kukiongoza kikosi hicho kwa mafanikio licha ya kuanza kwa kusuasua.
Imeripotiwa kuwa mapema leo hii mtendaji mkuu wa klabu hiyo Lee Congerton tayari alishawaandaa warithi wa mruguay huyo ili kuinusuru timu hiyo iliyopo katika ukanda wa kushuka daraja.
Kelvin Ball na Paul Bracewall ambao ni wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wameripotiwa kuwa mstari wa mbele kuchukua kiti hicho kwa muda mpaka pale watakapopata kocha mwingine.
Sunderland imeshinda mechi 4 tu katika ligi kuu nchini uingereza msimu huu na juzi wamepokea kichapo cha 4-0 kutoka wa Aston Villa kwenye uwanja wao wa nyumbani Stadium of Light huku mashabiki wa klabu hiyo kuonesha kuzidi kukasirishwa na mwenendo wa kocha huyo.
Matokeo hayo yaliipeka timu hiyo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 26 huku Burnley wakiwa nafasi ya 18 wakiwa na pointi 25 baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Manchester City katika mechi ya juzi jumamosi
0 comments:
Post a Comment