Monday, March 23, 2015



Na Bertha Lumala, Tanga
Polisi Morogoro FC iliyomtimua aliyekuwa kocha mkuu, Adolf Richard, imeshindwa kutamba mbele ya Tanzania Prisons FC baada ya timu hizo kutoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya jana jioni.

Mechi hiyo Na. 139 ya raundi ya 20 ya Ligi Kuu Tanzania Bara imeshuhudia Polisi Moro FC wakifikisha pointi 21 baada ya mechi 20 wakiendelea kusalia nafasi ya pili kutoka mkiani wakiwa na pointi sawa na Stand United FC walioko nafasi ya 11.

Prisons waliomtimua aliyekuwa kocha mkuu, David Mwamwaja, wameendelea kubaki mkiani wakifikisha pointi 17 baada ya mechi 19.

Timu mbili zitakazomaliza mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo, zitashuka daraja huku timu nne zilizofanya vizuri Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara msimu huu (FDL), Mwadui FC ya Shinyanga, Toto Africans ya Mwanza, Majimaji FC ya Ruvuma na African Sports ya jijini hapa zitapanda ligi kuu na kuifanya ligi hiyo kuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video