Monday, March 30, 2015

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi amefanya mazoezi na kikosi cha Simba jioni hii uwanja wa Chuo kikuu cha Dar es salaam kujiandaa na mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar itayopigwa mwishoni mwa wiki hii uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mbali na Okwi, Danny Sserunkuma ameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na kuonesha furaha ya kuendelea kuwepo Msimbazi. Pia Mganda mwingine, Joseph Owino amefanya mazoezi.
Simon Sserunkuma hajahudhuria mazoezi hayo na hayupo nchini.
Kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema vijana wake wanaendelea vizuri na wana uhakika wa kuchukua pointi tatu muhimu mbele ya Kagera Sugar.
"Tunaendelea na mazoezi vizuri, vijana wanapokea maelekezo vizuri, tutajitahidi kushinda dhidi ya Kagera". Amesema Kopunovic.
Mlinda mlango Hussein Sharrif 'Casillas' ameendelea kujifua kwa nguvu zote akishirikiana na kipa mkongwe Ivo Mapunda.
Kipa kinda Denis Richard walikuwa na ushirikiano mzuri na kipa mwenzake kijana Peter Manyika katika mazoezi hayo.
Wachezaji wengine walionesha morali kubwa wakiwemo Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Ibrahim Hajibu, Abdi Banda, Ibrahim Twaha, Mohamed Hussein, Elius Maguli, Masoud Nassor 'Cholo' na wengineo.
Hata hivyo, beki mahiri wa kulia, Hassan Kessy hajahudhuria mazoezi hayo kutokana na matatizo ya kifamilia.
Pia Juuko Mursheed hajafika katika mazoezi hayo na meneja wa Simba, Nico Nyangawa amesema bado yupo nchini Uganda kwa ruhusa maalumu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video