Kiungo mshambuliaji wa City, Peter Samson Mwalyanzi amesema hesabu zilizopo kwenye kikosi hivi sasa ni kushinda michezo yote mitatu inayokuja ambayo Mccfc itacheza ugenini ikianza na mchezo dhidi ya Ndanda Fc unaotarajiwa kuchezwa mkoani Mtwara mwishoni mwa juma lijalo.
Mwalyanzi aliyekwenye kiwango bora hivi sasa ameyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na mtandao huu mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya .
“City itakuwa nje ya Mbeya kwa michezo mitatu, dhidi ya Ndanda, Azam na Yanga, tumejiandaa vyema kuhakikisha tunapata matokeo kwenye michezo yote mitatu, watu wengi wanaweza wasiamini hili ninalosema lakini kwenye soka inawezekana, tunafahamu njinsi timu hizi zote zinavyocheza kwa kuwa tayari tushakuatana nazo naima tutafanikiwa kushinda zote tatu” alisema.
Akiendelea zaidi Mwalyanzi aliyefanikiwa kurudisha makali yake uwanjani baada ya kusota benchi kwa muda kufuatia majeraha aliyokuwa nayo aliweka wazi kuwa hivi sasa City iko kwenye kiwango kizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo hii ndiyo jambo pekee linalompa imani ya kuweza kuzikusanya poiti zote tisa dhidi ya timu hizo tatu.
“Michezo kadhaa iliyopita tulicheza tukiwa chini ya kiwango na hii ni kwa sababu wachezaji wengi ndani ya kikosi walikuwa majeruhi, kwa sasa ni tofauti kabisa, wote tuko safi na kila mmoja ana ari kubwa ya kucheza kwa mafanikio ili kupunguza kile kilichopotea mwanzoni mwa msimu ndiyo maana nikasema tunataka kushinda mechi zote tatu za nje” alimaliza.
0 comments:
Post a Comment