Mwamuzi wa kimataifa
wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi
ya AS Kaloum ya Guinea.
Katika mchezo huo wa
kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John
Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka
Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini
Afrika Kusini
Mchezo huo
unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia.
0 comments:
Post a Comment