Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Ikitoka nytuma ya goli 1-0, Brazil iliisambaratisha Ufaransa
kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopigwa usiku wa jana
Alhamis katika dimba la Stade de France. Kiungo mshambulizi, Oscar alifunga
goli la kusawazisha katika dakika ya 40 baada ya mlinzi wa Ufaransa, Raphael Varane kutangulia kuwafungia wenyeji
katika dakika ya 21. Neymar alifunga goli la pili dakika ya 57, kisha kiungo, Luiz Gustavo
akakamilisha hesabu baada ya kufunga bao la mwisho dakika ya 69.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa Brazil,
Carlos Dunga amesema kuwa ataendelea kuwekeza mbinu zake ili kuifanya timu hiyo
isipoteze uchezaji wake wa kawaida ‘ Samba’-Mchezo wa kupasiana huku wakimiliki
mpira na kuutawanya kila pembe ya uwanja.
Ufaransa ilijitahidi kumiliki mpira na kuibana Brazil. Timu
zote zilimaliza dakika 0 zikiwa na asilimia 50-50 za umiliki wa mpira lakini
vipaji zaidi vya Selecao ndivyo vilivyotoa tofauti kati ya ‘ Blues’ mabingwa wa
dunia, 1998 na washindi hao mara tano wa Kihistoria ambao walifanya vibaya
katika michuano iliyopita ya Kombe la dunia iliyopigwa Brazil- Brazuca 2014.
Neymar ndiye chache ya kikosi cha Dunga hivi sasa, akiwa
amefunga mabao nane katika michezo ya karibuni mchezaji huyo hupiga mashuti goli mara kwa mara.
Tfauti na ilivyokuwa ikicheza wakati wa utawala wa Big Phill, Dunga amefanya
mabadiliko makubwa katika kutoka timu ambayo ilichapwa mabao 7-1 na Ujerumani
katika nusu fainali ya kombe la dunia miezi tisa iliyopita.
Golikipa wa klabu ya Botofogo, Jefferson de Oliveira mwenye
miaka 32 amepewa jukumu la Julio Cesar, aliokoa nafasi sita kati ya saba ambazo
Ufaransa walizitengeneza katika mchezo huo na hadi sasa tayari amesaidia Brazil
kuhepeka kufungwa mara 13 tangu alipopewa nafasi na Dunga. Alionekana kujiamini
mbele ya washambuaji Karim Benzema na Antonio Griezmann.
Ni mchezaji mmoja tu kutoka katika kikosi cha kombe la dunia
aliyeanza katika idara ya ulinzi ( nahodha, Thiago Silva). Mlinzi wa FC Porto
ya Ureno, Danilo Luiz da Silva mwenye miaka 23 alianza katika nafasi ya mkongwe
Dan Alves. Dunga ameendelea kumtumia Filipe ‘ Luis’ Kasmirski kama mlinzi wa
kushoto mbele ya Marcelo.
Mlinzi huyo wa zamani
wa Atletico Mardid amecheza mara 12 tu msimu huu katika klabu ya Chelsea lakini
aliweza kuifanya Brazil kuwa imara zaidi katika upande wa kushoto. Mlinzi wa
kati, Joao De Souza Filho ‘ Miranda’ ameendelea kucheza kama mlinzi wa kati na
Brazil imekuwa ikicheza kwa nidhamu kubwa katika ulinzi tofauti na
ilivyoonekana katika Brazuca. Ufaransa ilimiliki mpira lakini haikuweza kupata
muda wa kutengeneza nafasi nyingi zaidi
ya nne za hatari walizopata.
SAFU IMARA YA KIUNGO…
Dunga alishuhudia timu yake ikiruhusu mipira ya kona mara
saba, hili ni eneo ambalo Ufaransa huwamaliza Brazil mara kwa mara, mwaka 1998
katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia, kiungo Zinedine Zidane ‘ Zizzou’
alifunga mara mbili kwa mipira ya kichwa, Brazil ikachapwa tena na Ufaransa kwa
stahili ya mipira ya kona katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya mabingwa
wa Mabara wa FIFA mwaka 2001.
Mwaka, 2006, Thierry Hennry aliwaondoa kwa bao la
kichwa katika mchezo war obo fainali ya kombe la dunia akiunganisha mpira wa
faulo za Zidane. Imekuwa hivyo tena kwa Varane, lakini bado Dunga anaweza
kusema tena kwa kujiamini kuwa ‘ mpira alisi wa Brazil hautapotea chini yake’
. Selecao walitengeneza nafasi 15 katika
dakika zote 90 huku nane zikiwa za hatari. Golikipa, Steven Mandanda ali-save
mara kumi timu yake.
Gustavo, Willian, Oscar na Elias walicheza vizuri katika
eneo la kiungo, wakiwa nguvu katika kuzuia na maarifa katika kushambulia. Dunga
alimpa uhuru kiungo wa Corinthians, Elias kuichezesha timu sambamba na Oscar
ambao walisaidiwa jukumu hilo la Neymar. Brazil ilikuwa imara katikati ya
uwanja na Dunga a;likuwa na wachezaji wa kutosha katika benchi kama Douglas
Costa, Fernandinho, Marcelo, Souza , Luiz Adriano ambao waliingia uwanjani
katika muda tofauti ndani ya dakika saba za mwisho. Unapoona mchezaji mwenye
kipaji kama Phillipe Coutinho akikosa walau dakika moja ya kucheza bila shaka
ni kielelezo tosha kuwa timu hiyo bado ina utitiri wa vipaji.
Neymar ameendelee kufunga mabao chini ya Dunga nap engine
kijana huyo anawea kuendelea kuwa ‘ funguo’ mpya ya soka la Brazil akiwa
sambamba na Luis Adriano, Robinho De Souza, Roberto Firmino. Kitendo cha
kyuishinda Ufaransa huku wakimaliza mechi na faulo 13 bila kadi yoyote ni
ishara nje kuwa nidhamu ya kaiwada ya wachezaji ndani ya uwanja imerejea na
Dunga ni mtu anayependa kusimamimia jambo hilo kwa uzito mkubwa. Brazil imekuwa
ikicheza kitimu zaidi kwa sasa na hilo linafanya wawe wagumu mno uwanjani.
0 comments:
Post a Comment