Kikosi cha Simba SC kimetinga jijini Tanga tayari kwa mechi yao inayofuata dhidi ya Mgambo Shooting Stars.
Simba SC ambayo kwa sasa inatambia mabao ya 'mzimu' ya kiungo wao mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi, watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Mgamb o Shooting Stars ya Tanga watakapopambana katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani jijini humo Jumatano.
Kwa mujibu wa kocha msaidizi, Suleiman Matola, kikosi cha Simba SC kimeanza safari kuondoka jijini hapa jana majira ya saa tano asubuhi.
Mgambo Shooting Stars inayonolewa na Bakari Shime, huwa na utaratibu wa kukaza kwa kuhakikisha haipotezi mechi za mzunguko wa pili, hasa zinazochezwa Uwanja wa nyumbani, Mkwakwani.
Haijawahi kufungwa na Yanga SC wala Simba SC kwenye Uwanja wa Mkwakwani tangu ipande ligi kuu msimu miwili iliyopita.
Msimu uliopita iliifunga Simba 1-0 kisha ikaipiga Yanga SC 2-1 kwenye uwanja huo.
0 comments:
Post a Comment