Friday, March 20, 2015

MBEYA CITY FC itasafiri kwenda mkoani Mtwara kuchuana na Ndanda fc katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara itayopigwa aprili 4 mwaka huu uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Tayari kikosi cha City chini ya kocha Juma Mwambusi aliyeripotiwa kuwa hatarini kutimuliwa kabla ya kuifunga 2-0 Stand United kimeanza maandalizi ya mechi hiyo ili kuendelea kujikita nafasi nzuri zaidi katika msimamo.
IMG_0019
Ushindi dhidi ya Stand umewafanya Mbeya City kupanda mpaka nafasi ya 9 wakijikusanyia pointi 23 kibindoni baada ya kushuka dimbani mara 19.
Katika mechi 19 walizocheza msimu huu, City wameshinda mechi 5, sare 8 na kufungwa mechi 6 tofauti na msimu uliopita waliofungwa mechi tatu tu dhidi ya Yanga (1-0), Coastal Union (2-0) na Azam fc (2-1).
Pia City wamefunga magoli 14 na kufungwa 16, hivyo tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni -2.
IMG_0063
Kuelekea mechi dhidi ya Ndanda, kocha Juma Mwambusi amewashukuru vijana wake kwa kupambana na kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Stand United, huku akiwataka kujiweka tayari kwa mchezo unaofuata mkoani  Mtwara.
“Tulicheza vizuri, nashukuru kwa jinsi tulivyopambana mpaka tukapata ushindi, hizi ni pointi tatu muhimu ambazo zimetusogeza kwenye nafasi nyingine kwenye msimamo wa ligi, kikubwa tujiandae na tuwe tayari kwa kupambana zaidi kwenye mchezo ujao dhidi ya Ndanda ambao tutacheza ugenini huko Mtwara” alisema Mwambusi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video