Tuesday, March 31, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mtibwa Sugar FC na Kagera Sugar zilitoka sare ya 1-1 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwa siku mbili kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Km 100 kutoka mjini Mrogoro Januari 8-9, mwaka huu, wenyeji wakifunga bao siku ya kwanza kabla ya wageni kusawazisha siku ya pili.

Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar FC, Mecky Mexime, ametamba kuwa amekisuka vizuri kikosi chake ili kuwafunga ndugu zao Kagera Sugar FC katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa usukumani kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Akiwa mjini Shinyanga leo mchana, Mexime, nahodha wa zamani wa Taifa Stars na Mtibwa Sugar FC, amesema kikosi chake ambacho kilifungwa 1-0 dhidi ya Simba SC jijini hapa katika mechi iliyopita ya ligi hiyo, kiko kamili na kinasubiri muda ufike kusaka pointi tatu dhidi ya timu hiyo iliyoko nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25, mbili mbele ya Mtibwa walioko nafasi ya nane.

"Tupo hapa Shinyanga tangu juzi (Jumapili) kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Kagera. Tumejiandaa vyema ili tupate pointi hapa maana msimu huu ni mgumu. Tumekuja na wachezaji 20 na wote wana hali nzuri kiafya," ametamba Mexime.

Kocha mkuu wa Kagera Sugar FC, Mganda Jackson Mayanja, amesema nyota wake wanaoongozwa na mkali wa mabao Rashid Mandawa, wako tayari kupambana na wakatamiwa wenzao huku akitabiri kuwa mechi itakuwa ngumu kutokana na ubora wa kikosi cha wapinzani wao.

"Mtibwa ni moja ya timu nzuri na ngumu kufungika, itakuwa mechi ngumu, lakini tumejipanga kupata matokeo mazuri nyumbani," amesema kocha huyo.

Kagera Sugar FC ambayo ilifungwa 2-1 dhidi ya Yanga SC katika mechi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini hapa, imepoteza mechi moja kwenye Uwanja wa CCM Kambarage tangu ihamishie maskani yake mjini Shinyanga miezi miwili iliyopita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video