Wednesday, March 18, 2015


Simba waliposhinda 1-0 dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Taifa mwaka 2013

Na Bertha Lumala
Kocha mkuu wa Mgambo Shooting Stars, Bakar Shime, amesema kuwa kuelekea mechi yao ya leo dhidi ya Simba SC, hawaangalii rekodi za klabu hiyo ya Msimbazi na makali ya kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi.

Simba SC ina kibarua kigumu mbele ya 'maafande' hao kutoka kitongoji cha Kabuku wilayani Handeni, Tanga timu hizo zitakapochuana katika mechi ya kiporo ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo jioni.

Mechi hiyo Na. 62 ya raundi ya 9 ya Ligi ya Bara, ilipaswa kuchezwa Januari 4, lakini ikapigwa kalenda na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na ushiriki wa Simba SC katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwanzoni mwa mwaka.

Akiwa jijini Tanga leo asubuhi, Shime ameuambia mtandao huu kuwa kikosi chake kiko tayari kukabiliana na Simba SC na kulinda rekodi yao ya kutopoteza mechi hata moja dhidi ya timu kongwe nchini Simba SC na Yanga SC Uwanja wa Mkwakwani tangu kipande ligi kuu misimu miwili iliyopita.

Amesema Simba SC ina kikosi kizuri kilichoshinda mechi tatu mfululizo tangu kifungwe 1-0 dhidi ya Stand United FC usukumani mjini Shinyanga, lakini haikihofii kwa sababu timu yake nayo ina rekodi nzuri ikiwa imepoteza mechi moja tu katika mechi nne zilizopita.

"Tuna wachezaji 22 ambao wote wako tayari kwa mechi ya leo, ni kuchagua tu acheze nani. Tumefuatilia mechi za Simba, wameimarika ingawa mabao yao katika mechi mbili zilizopita yalifungwa pasipo kutarajiwa.

"Tuna rekodi nzuri hapa Tanga dhidi ya Simba SC, lakini leo hatutazizingatia. Itakuwa vita ya dakika 90 ya Mgambo dhidi ya Simba bila kujali kipindi cha nyuma kulitokea mambo yepi," amesema Shime.

Goran Kopunovic, kocha mkuu wa Simba SC, amesema mechi ya leo itakuwa ngumu kwa kikosi chake kutokana na ubovu wa Uwanja wa Mkwakwani, lakini watapambana ili washinde.

Amesema tangu atua Msimbazi na kusaini mkataba wa miezi 6, amebaini kuwa timu 'ndogo' zimekuwa zikikamia timu yake hasa inapocheza nje ya Dar es Salaam.

Simba SC wanaotambia makali ya Mganda Okwi kwa sasa, wanasaka ushindi leo ili kulipa kisasi cha kufungwa na Mgambo Shooting Stars jijini Tanga msimu uliopita wakati timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nayo ikisaka kisasi cha kufungwa na Simba mabao 6-0 jijini Dar es Salaam msimu uliopita.
 
Wanamsimbazi leo pia watakuwa na mshambuliaji wao wenye 'hat-trick' pekee Ligi Kuu ya Bara msimu huu, Ibrahim Ajibu, anayerejea uwanjani baada ya kukosa mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuwa na kadi nne za njano.

Mgambo huwa haipotezi mechi kirahisi mzunguko wa pili kwenye uwanja wa nyumbani. Msimu uliopita ilichukua pointi zote 6 dhidi ya Simba SC (1-0) na Yanga SC (2-1) Uwanja wa Mkwakwani, pointi ambazo ziliinusuru kuporomoka daraja.

Msimu wa 2012/13 Mgambo Shooting Stars ilitoka suluhu dhidi ya Simba SC kabla ya kuinyuka timu hiyo bao 1-0 msimu uliopita.
Simba SC iko nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 29 baada ya mechi 18 wakati Mgambo iko nafasi ya 10 ikiwa na pointi 21 baada ya mechi 17.

Mechi nyingine za leo ni Yanga SC (walioko nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 31, mbili nyuma ya vinara Azam FC) dhidi ya Kagera Sugar FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Mbeya City FC watakuwa wenyeji wa Stand United FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video