MECHI ya kimataifa ya kirafiki baina ya wenyeji Simba SC na Bata Bullets ya Malawi iliyopangwa kuchezwa leo jioni saa 10:00 uwanja wa kimataifa wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam imefutwa.
Taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji zinaeleza kuwa kuna mambo yameingiliana, hivyo mashabiki hawataweza kushuhudia mechi hiyo iliyopangwa kuoneshwa na Azam TV.
Kipute hicho kilitakiwa kuchezwa jana jioni, lakini kiliahirishwa mpaka leo na leo kimefutwa kabisa.
Simba wameamua kusubiri mechi yao ya ligi kuu mwishoni mwa wiki dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Taifa.
Mnyama ataingia katika mechi hiyo akiwa na kumbukumbu ya kushinda 1-0 dhidi ya watani zake wa jadi, Dar Young Africans.
0 comments:
Post a Comment