KUELEKEA mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara kati ya City na Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Manungu Complex jumapili hii, Kocha mkuu wa kikosi cha Mbeya City Juma Mwambusi amesema nyota wa kikosi chake wako tayari kwa mchezo huo .
Mwambusi ameuambia mtandao huu kuwa kuwa hesabu zote kuelekea mchezo huo zimekamilika hasa baada ya kurejea na kuanza kufanya mazoezi kwa nyota ambao waliapata majereha kwenye michezo miwili iliyopita.
“Tumecheza michezo miwili hapa Sokoine, dhidi ya Yanga na Ruvu Shooting, dakika 180 za mechi hizo mbili zilifanya tuwe na majeruhi zaidi ya watatu kikosini, Nashukuru Mungu kuwa sasa wamerejea na tayari wameanza mazoezi mepesi, tunaamini siku hizi mbili watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa jumapili hii inamaana kuwa hesabu zimekamilika” alisema.
Katika hatua nyingine daktari mkuu wa City, Dr Joshua kaseko amethibitisha kupona majereha kwa nyota watatu walikuwa hatihati kucheza jumapili kufuatia kuumia kwenye michezo iliyopita.
“Waliumia lakini sasa wamepona na leo wameanza mazoezi, Stive Mazanda, John Kabanda, na Mwegane Yeya walikuwa kwenye hatihati ya kucheza mchezo ujao lakini tunashukuru kuwa wamepona na tunaamini siku ya mchezo watakuwa kamili kucheza dakika zote 90″ alisema Dr Kaseko.
0 comments:
Post a Comment