Wednesday, March 18, 2015



Na Bertha Lumala
Wagonga nyundo wa Jiji la Mbeya, Mbeya City FC, wameutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuichapa Stand United FC mabao 2-0 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo jioni.

Mabao ya Yusuf Abdallah aliyefunga kwa penalti dakika ya 65 na Paul Nonga katika dakika ya 75, yalitosha kupeleka kilio kwa timu hiyo ya usukumani mjini Shinyanga ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo na kuacha pointi zote sita Uwanja wa Sokoine baada ya Jumapili kuchapwa 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Kwa ushindi huo, Mbeya City FC inayonolewa na kocha bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Juma Mwambusi, amekwea kutoka nafasi ya 12 hadi nafasi ya 7 wakifikisha pointi 24 sawa na Coastal Union waliopo nafasi ya 6.

Stand walioshinda mechi tatu mfululizo uwanja wao wa nyumbani kabla ya kwenda Mbeya, wameporomoka kutoka nafasi ya 7 waliyokuwapo kabla ya kutinga jijini Mbeya hadi nafasi ya 12 wakiwa na pointi 22 baada ya mechi 20.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video