JAMANI! Arsenal 'Bai Bai' ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kutupwa nje kwa wastani wa mabao 3-3, lakini bao la ugenini walilovuna Monaco mjini London limewapeleka mbele.
Usiku huu, Arsenal wameshinda mabao 2-0 dhidi ya Monaco katika mechi ya marudiano ya hatua ya 16 ya ligi ya mabingwa, mabao yakifungwa na Olivier Giroud dakika ya 36' na Aaron Ramsey dakika ya 79'.
Mechi ya kwanza uwanja wa Emirates Arsenal walifungwa 3-1.
Licha ya kutolewa, Arsenal wameonesha kandanda safi na kwa dakika 90 wamemiliki mpira kwa asilimia 62 kwa 38.
Pia walifanikiwa kupiga mashuti 8 yaliyolenga lango, wakati Monaco hawakupiga shuti lolote.
Arsenal ni timu ya pili ya Uingereza kutolewa ligi ya mabingwa na walianza Chelsea.
Mechi ya kwanza ugenini, Chelsea walitoka 1-1 na PSG na mechi ya pili wakatoka sare ya 2-2.
Ingawa wastani ulikuwa 3-3, mabao mawili ya ugenini dhidi ya moja la Chelsea la ugenini, yakawavusha PSG robo fainali ya UEFA msimu huu.
Sasa matumaini ya Waingereza yamebakiwa kwa Manchester City ambao leo jumatano wanakabiliana na FC Barcelona katika mchezo wa marudiano uwanja wa Camp Nou.
Mechi ya kwanza Etihad, City walichapwa 2-1 na wahaitaji ushindi wa mabao 2-0 ili kusonga mbele moja kwa moja.
Wakishinda 1-0 watatolewa kwa goli la ugenini kwani tayari Barca walishafunga mawili ugenini.
0 comments:
Post a Comment