Tuesday, March 17, 2015

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania Francis Cheka aliefungwa jela miaka mitatu kwa kosa la kushambulia na kudhuru mwili leo hii amebadilishiwa kifungo kutoka kifungo cha jela na kuwa kifungo cha nje.
Bondia huyo alifungwa jela Februari 3 mwaka huu na hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa meneja wa bar yake aitwaye Bahati Kibanda.
Akizungumza kutoka mjini Morogoro mwenyekiti wa huduma za jamii mkoani Morogoro (Parole) waliofanikisha zoezi hilo Yusuph Ponera amesema walifuatilia rekodi za bondia huyo kutoka mtaani kwake na kubaini kuwa hakuwa na rekodi yoyote ya makosa ya jinai na ndipo alipounganishwa katika idadi ya wafungwa waliohitaji kubadilishiwa kifungo.
Kwa mujibu wa mapromota wa ngumi Cheka anatarajiw kupanda ulingoni mwezi May mwaka huu kutetea ubingwa wake wa WBF uzani wa kati dhidi ya bondia atakayejulikana baadaye.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video