"Tuliwaahidi washabiki wa Yanga FC kuwapa faraja kwa kuwafunga Simba katika mchezo wetu wa ligi kuu ya vodacom Machi 22, 2015, uwanja wa taifa ahadi ambayo hatukuitimiza baada ya kufungwa bao 3-0.
Dhamira yetu ilikuwa ni hiyo ya kuwafunga Simba lakini ikishindikana kwasababu ya sababu zilizojitokeza!.
Nitumie fursa hii kuwataka radhi washabiki wa Yanga ambao tunaamini walikuwa nyuma yetu wakitushangilia ili kuwapa nguvu vijana wetu kwa lengo la kuwawezesha wafanye vizuri lakini ikashindikana!
Vijana wetu walijitahidi kufanya vema japo nakiri hawakucheza kwa kiwango kile tunachokifahamu!
Mwamuzi wa mchezo wa jana aliwadhoofisha vijana wetu kwa kutoa penalti ambayo tunadhani haikuwa sahihi!
Baada ya penalti hiyo tulifungwa bao la haraka la pili kutokana na hisia za vijana kukata tamaa na maamuzi ya mwamuzi.
Ahsante Yanga kwa kutuunga mkono japo tumewaangusha. Hatukupenda iwe hivyo bali ni mapenzi ya Mungu ambaye tunadhani hakupenda tupate ushindi!
Jana kabla ya mchezo nilitabiri kwamba mchezo utakuwa na mabao matatu, na kweli yakawa matatu kwa sisi kufungwa!
Niliota usiku wa kuamkia mchezo tukiwa tumeshinda 2-1 lakini hali ikiwa tofauti. Wenzetu waligeuza matokeo ya ndoto yangu, yale mawili ya kwetu wakayachukua wakaongeza katika lao moja yakawa matatu!
Hongereni Simba kwa ushindi japo...."
0 comments:
Post a Comment