Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester City ambae kwa sasa anainoa Intermilan Roberto Mancini amesema anaamini kuwa kiungo mchezeshaji wa klabu ya manchester city Raia wa Ivory Coast Yaya Toure atajiunga na miamba hao wa soka wa Nchini Italia baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia ya kuondoka katika dimba la Etihad msimu ujao.
Yaya ambaye amekuwa na kiwango kibovu tangu aipe timu yake ya Ivory Coast ushindi na kutwaa kombe la Mataifa Barani Afrika sasa huenda njia yake ikawa nyeupe kutoka Manchester City, baada ya kutua kwa viungo kama vile Fernando pamoja na Fernandinho.
0 comments:
Post a Comment