MABINGWA watetezi wa ligi kuu England, Manchester City baada ya kutolewa na Barcelona katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wamehamishia hasira zao kwenye michuano ya EPL.
Jioni ya leo wakiwa nyumbani Etihad mjini Manchester wameivurumishia West Bromwich Albion mabao 3-0 katika mechi ya ligi.
Matokeo hayo yamewaweka City nafasi ya pili kwa pointi 41, tatu nyuma ya vinara Chelsea.
Mapema dakika ya 2' Gareth McAuley alioneshwa kadi nyekundu na Muamuzi Neil Swarbrick na kuwaacha wenzake kucheza pungufu kwa zaidi ya dakka 88'.
City walitumia mapungufu hayo kwa kufunga magoli matatu kupitia kwa Wilfried Bonny dakika ya 27, Fernando dakika ya 40' na David Silva dakika ya 77.
Chakufurahisha zaidi kwa dakika 90' zote City walipiga mashuti 16 yaliyolenga lango wakati West Brom hawakupiga shuti lolote.
City walimiliki mchezo wa asilimia 79 dhidi ya 21 za wapinzani wao.
Kiujumla vijana wa Pellegrini walikuwa bora kwa kila kitu leo hii.
Mechi nyingine za EPL zinaendelea muda huu na matokeo yote utapata hapa hapa.
MSIMAMO BAADA YA CITY KUSHINDA
0 comments:
Post a Comment