Baada ya klabu ya Manchester United kupwaya katika nafasi ya kiungo siku za hivi karibuni, klabu hiyo chini ya kocha Mholanzi Louis Van Gaal yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford, ipo mbioni kumfukuzia kiungo wa klabu ya Borrusia Dortmund Ilkay Gundogan.
Gundogan ambaye amekuwa akifanya vizuri katika mechi za karibuni akiwa na klabu yake ya Dortmund sasa ameonekana Lulu kwa Manchester United huku klabu hiyo ikifanya jitihada za kumpeleka Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment