Rais
wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za
pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na
ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata
Twiga Stars katika mchezo huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri
waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na
TFF.
Aidha Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo
wa awali walioupata, bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo
wa marudiano ili waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa
ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April
10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa
moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women)
zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku
(jumanne) jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia
ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa pongezi Twiga Stars kwa
ushindi walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa
marudaiano.
Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia
(The She-polopolo) yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na
Sophia Mwasikili (1).
0 comments:
Post a Comment