Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema pangua pangua ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu imelitia doa shirikiho hilo, na wanajipanga kuhakikisha fadhaa hiyo haitokei tena.
Malinzi ameuambia mtandao huu jijini hapa leo kuwa mara tu baada ya kumalizika kwa msimu huu waLigi Kuu Tanzania Bara Mei 9, mwaka huu, vyombo vya TFF (Kamati ya Mashindano na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania - TPLB) vitakutana na kupanga ratiba makini ya msimu ujao.
"Ratiba ya Ligi Kuu Tanzamnia Bara msimu huu umetia toa. Tulifanya makosa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ratiba yetu haikujali michuano hiyo. Msimu ujao tutahakikisha tunakuja na ratiba itakayojali matukio yote ya soka yakiwamo mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ratiba ya Taifa Stars na Taifa Stars Maboresho maana programu ya maboresho ni ya kudumu," amesema Malinzi.
TFF imefanya marekebisho makubwa ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu mara tatu. Ligi hiyo ilipaswa kuanza Agosti 24, mwaka jana lakini ikapanguliwa hadi Septemba 20 kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi hata hivyo.
Mabadiliko ya pili yalifanywa mwanzoni mwa Oktoba mechi za raundi ya nne zilizokuwa zichezwe Oktoba 12 zikapigwa kalenda hadi Oktoba 18 kupisha mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyokuwa kwenye kalenda ya FIFA ya Taifa Stars dhidi ya Benin.
Mabadiliko mengine makubwa yaliyosababisha kuvurugika kwa kiasi kikubwa kwa ratiba ya ligi hiyo yalianza kufanywa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar Januari 13.

0 comments:
Post a Comment