Kocha wa klabu ya Manchester United Mholanzi Loius Van Gaal, amemshutumu mchezaji wake Raia wa nchini argentina Angel Di Maria kwa kadi nyekundu ya kizembe aliyopewa hapo jana dhidi ya arsenal katika mchezo wa kombe la FA lililopigwa katika dimba la Old Trafford na Arsenal kuweza kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Di Maria alizawadiwa kadi ya pili ya njano na kupewa kadi nyekundu baada ya kumvuta shati mwamuzi licha ya mwamuzi huyo kumuacha baada ya kujiangausha nje ya kumi na nane ya goli la Arsenal.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa akitokea katika klabu ya Real Madrid sasa ataukosa mchezo unaofuata wa ligi kuu Nchini Uingereza dhidi ya klabu ya tottenham hotspurs katika dimba la Old Trafford wikiendi ijayo ambapo United watakuwa wanasaka pointi tatu muhimu katika mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment