Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kocha mkuu wa AFC Leopards, Zdravko Logarusic amesema anawachukulia wachezaji wote wa klabu hiyo kama nyota wapya.
Mcroatia huyo aliyeteuliwa na Ingwe wiki mbili zilizopita akirithi mikoba ya Mdachi, Pieter De Jongh ambaye amefukuzwa.
Logarusic amenukuliwa na mtandao rasmi wa klabu hiyo leo akieleza kuwa atawapa nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwake kwa kuwa anaamini kila mchezaji kwa kocha mpya ni sawa na mchezaji anayesajiliwa katika klabu mpya.
Ninawachukulia wachezaji wote kama wachezaji wapya waliosajiliwa, ni jukumu la kila mmoja kuonesha uwezo wake," amesema Loga.
Ingwe ya kocha huyo wa zamani wa Simba, Loga, ilishikwa 0-0 dhidi ya Chemelil Sugar katika mechi yao ya kwanza ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) iliyochezwa Jumapili.

0 comments:
Post a Comment