Kocha mkuu wa AFC Leopards FC ya
Ligi Kuu ya Kenya, Zdravko Logarusic ameponda mfumo wa klabu nyingi za
nchi hiyo kucheza kwa kujilinda badala ya kushambulia akidai kuwa
kunarudisha nyuma maendeleo ya soka la Kenya.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu hiyo muda mfupi baada ya timu yake kulala 1-0 dhidi ya Ulinzi Stars, Logarusic amesema muda mwingi wakati wa mechi hiyo kulikuwa na tabia za kupoteza muda wapinzani wao kutangulia kupata bao.
Ameongeza kuwa timu yake bado ni mbovu na anapaswa kufanya mabadiliko makubwa ya wachezaji wakati wa usajili wa katikati ya msimu.
"Soka la Kenya halitakua kama timu zikishafunga goli moja kisha zinaacha kucheza kwa muda wote wa mechi uliobaki (kipigo cha 1-0 dhidi ya Ulinzi Stars). Kulikuwa na kupoteza muda kwingi wakati wa mechi na refa alipaswa kuongeza muda mwingi zaidi.
Wachezaji mizigo
"Hata hivyo, hatukufunga hivyo hatukustahili kushinda mechi. Pia nimebaini kuna mizigo mingi ndani ya klabu, lakini ninashukuru kwa sababu imebaki miezi mitatu kabla sijafagia nyumba."
Kipigo dhidi ya Ulinzi ni cha kwanza kwa bosi huyo mpya wa Leopards tangu ajiunge nao mapema mwaka huu. Ingwe kwa sasa iko nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya Kenya ikiwa na pointi saba baada ya mechi nne.
Timu hiyo ya kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia FC ya Kenya na Simba SC ya Tanzania, itakuwa mgeni wa Thika United FC katika mechi inayofuata ya ligi hiyo.

0 comments:
Post a Comment