Geilson Santos Santana 'Jaja' alikuwepo mechi iliyopita Kaitaba, Yanga ikinolewa na Marcio Maximo
KATIKA mechi 5 za mwisho walizocheza Yanga, wamecheza mechi 3 za ligi na 2 za kimataifa.
Katika mechi 3 za ligi wameshinda mbili, 3-0 dhidi ya Prisons na 3-1 na Mbeya City fc katika uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya. Wamefungwa 1-0 na Simba uwanja wa Taifa.
Kabla ya kucheza na Simba walikwenda Botswana na kufungwa 2-1 na BDF XI katika mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho, lakini walisonga mbele kwa wastani wa mabao 3-2 kwani mechi ya kwanza uwanja wa Taifa, Dar es salaam walishinda 2-0.
Baada ya kuwatoa BDF walitakiwa kucheza mechi ya ligi machi 11 dhidi ya JKT Ruvu kabla ya kuwavaa FC Platinum machi 15, lakini waligomea mechi hiyo na mwishoni mwa wiki iliyopita walishinda 5-1 dhidi ya Platinum katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho.
Leo Yanga wanacheza na Kagera Sugar uwanja wa Taifa, je, wataendeleza makali yao?
Kwa upande wa Kagera Sugar mechi 5 zilizopita wameshinda 3, wamefungwa 1 na sare 1.
Waliwafunga Mgambo JKT 1-0, wakawafunga 1-0 JKT Ruvu, wakawalaza 1-0 Polisi Moro kabla ya kufungwa 2-0 na Stand United, mechi zote zilipigwa uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Baada ya kipigo hicho wakasafiri kwenda Tanga na kutoa sare ya 2-2 na Coastal Union uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Je, rekodi nzuri ya ushindi wataendeleza mbele ya Yanga? kumbuka mechi ya kwanza kaitaba waliwafunga Yanga 1-0.
0 comments:
Post a Comment