Klabu ya Yanga imetangaza viingilio vya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe huku kiingilio cha chini kikiwa ni Sh. Sh.5,000 na cha juu Sh.30,000.
Mechi kati ya timu hizo itapigwa Uwanja wa Taifa Jumapili na FC Platinum ilitarajiwa kutua jijini hapa leo saa moja usiku tayari kwa mtanange huo.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro, ameuambia mtandao huu kuwa viingilio vitakuwa VIP A Sh. 30,000, VIP B Sh. 25,000, VIP C Sh. 20,000 viti vya rangi ya chungwa Sh.10,000.
Marefa wa mechi hiyo wanatoka Djibouti huku kamishna akitokea Malawi na watawasili kesho jijini hapa.
0 comments:
Post a Comment