CHELSEA, Tottenham leo usiku majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki zinachuana uwanja wa Wembley, mjini London kusaka bingwa wa kombe la ligi 'Capital One Cup'.
Kuelekea katika mechi hiyo, kocha mwenye maneno mengi na mjanja wa kucheza na akili za makocha wenzake, Jose Mourinho amesema kama asingeweza kuifundisha Tottenham kwa heshima ya mashabiki wa Chelsea.
Mourinho amesema wapinzani wao wa fainali ya Capital One walijaribu kumchukua mwaka 2007 alipoondoka Chelsea.
Mourinho alishawishiwa kujiunga na Spurs na mmiliki wa klabu hiyo, Daniel Levy baada ya Mourinho kuachana na Chelsea kwa makubaliano maalumu kufuatia kutoelewana na bodi ya wakurugenzi na mmiliki wa timu Roman Abramovich.

Daniel Levy
Lakini asingeweza kukubali kuifundisha Tottenham kwasababu kwa wakati huo alikuwa amesaini makubaliano kuwa hawataweza kufundisha klabu nyingine ya England kwa miaka miwili zaidi baada ya kuachana na Chelsea na amesema asingefanya hivyo kwasababu ana mahusiano mazuri zaidi na Chelsea.
Aliulizwa kama Spurs walimfuata 2007, alisema: "Ndiyo. Nisingeweza kwenda. Sikutakiwa kufundisha England kwa miaka miwili".
Kwa mujibu wa Mourinho Tottenham walijaribu kuzungumza na Chelsea ili kuvunja kipengele hicho cha mkataba cha kumzuia kufanya kazi England,lakini pia alisema; "Nisingekubali kazi hiyo kwasababu nawapenda sana mashabiki wa Chelsea"
0 comments:
Post a Comment