Friday, March 20, 2015



Na Bertha Lumala, Tanga
Kocha mkuu wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic, amesema timu yake ilizidiwa na Mgambo Shooting Stars katika mechi yao ya juzi ya kiporo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikiwa imeshinda mechi tatu mfululizo na kuinua matumaini ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu ya  Bara msimu huu, Simba SC ilijikuta ikifunzwa soka na kuchapwa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting Stars Uwanja wa Mkwakwani.
Msemaji mpya wa Simba SC, Hajji Manara, ameuambia mtandao huu kuwa kocha wao huyo amewataka kusahau yaliyotokea jijini hapa jana ili wajiandae vyema kwa mechi ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Ruvu Shooting Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

"Kocha mkuu (Goran) amesema timu yake ilishindwa kufanya vyema dhidi ya Mgambo kutokana na ubovu wa uwanja. Amesema ni matokeo ya mpira, hivyo tunapaswa kuyapokea maana kuna kushinda, kufungwa na sare. Timu tayari imesharejea Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya Ruvu Shooting," amesema mtoto huyo wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Sunday Manara.

Aidha, mara tu baada ya kumalizika kwa mechi hiyo jijini hapa juzi, nahodha wa Simba SC, Hassan Isihaka, alisema timu yao ilizidiwa mbinu na wenyeji wao.

"Kwa kweli Mgambo wamecheza vizuri na kutufunika hasa safu ya kiungo. Safu yao ya ulinzi pia ilikuwa imara na haikufanya makosa mengi kama tuliyofanya sisi (Simba). Tunapaswa kuyakubali na kuyapokea matokeo haya na kujipanga kwa mechi zinazofuata," alisema Isihaka.

Simba SC iliyolazimika kucheza pungufu kwa mchezaji mmoja kuanzia dakika ya 68 baada ya kipa wake mkongwe, Ivo Mapunda kutolewa kwa kadi nyekundu na refa Amon Paul wa Mara, ilizidiwa kwa kiasi kikubwa na Mgambo katika mechi ya jana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video