SIMBA SC wameanza mazoezi wakijiandaa na mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar itayopigwa uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga, Aprili 4 mwaka huu.
Katika mazoezi ya jana jioni uwanja wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kocha Goran Kopunovic aliendelea kuwapa mazoezi ya kuongeza kasi na kumiliki mpira.
Hassan Isihaka, Said Ndemla na Abdi Hassan Banda hawakudhuria mazoezi hayo kwasababu wapo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyoweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki ya FIFA dhidi ya Malawi itayopigwa uwanja wa CCM Kirumba, machi 29 mwaka huu.
"Nimeanza mazoezi ya kuwakabili Kagera, waliifunga Simba wakati huo ukiwa na kocha mwingine, Simba ya sasa ni mpya, kocha Goran ni tofauti na aliyepita, naenda Shinyanga kutafuta ushindi". Amesema kocha Kopunovic.
"Kagera ni washindani wazuri, lolote linaweza kutokea, lakini tunajiandaa vizuri sana na tunaamini tutafanya vizuri".
0 comments:
Post a Comment