Saturday, March 21, 2015

KWA takribani miaka mitano sasa kutoka mwaka 2010, Ruvu Shootings haijawahi kuifunga Simba SC katika mechi 9 za ligi kuu walizochuana.
Simba wameshinda mara 8 na walitoka sare ya 1-1 mara moja na hii ilikuwa Oktoba 5 mwaka 2013.
Hata msimu huu, Simba chini ya Patrick Phiri ilivuna pointi tatu kwa mara ya kwanza dhidi ya Ruvu Shootings, raundi ya 7 ikishinda 1-0 uwanja wa Taifa novemba 9 mwaka jana. Bao pekee likifungwa na Emmanuel Okwi.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya 10 kesho majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Taifa kutoka mwaka 2010 na tayari kocha mkuu wa Simba Goran Kopunovic ameshatamka maneno mazito.
Kopunovic mwenye machungu ya kufungwa 2-0 na Mgambo JKT uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga jumatano ya wiki hii amesema:
"Timu yangu ni nzuri, ina wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu mfano Okwi (Emmanuel) ana maajabu makubwa ya soka hasusani mabao anayofunga. Tulianguka dhidi ya Mgambo, walikuwa bora siku hiyo na walituzidi ujanja, lakini mpira wa miguu uko hivyo, kuna wakati unafanya vizuri kuna wakati unaanguka"
"Mimi na Matola tunajitahidi sana kuiboresha timu, kesho tunaamini tutafanya vizuri, niwaambie mashabiki wa Simba, tunafanya kazi kwa asilimia 100 kuisaidia timu, hatujakata tamaa na wao waendelee kutushangilia". 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video