Monday, March 9, 2015

Kiungo wa klabu ya Juventus Federico Mattiello anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Chievo amevunjika mguu baada ya kuchezewa rafu mbaya na kiungo wa AS Roma Radja Nianggolan  katika mechi ya Serie A iliyozikutanisha timu hizo hapo jana kwenye uwanja wa San Antonio Bentegodi .
Tukio hilo ambalo lilitokea katika dakika ya 16 ya mchezo liliteka hisia za watu wengi walioshuhudia mchezo huo na pia lilipelekea wachezaji wa timu zote mbili kupunguza kasi ya mchezo kwa kuhofia kuumia.
Baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 kupatiwa huduma ya awali baadaye alitolewa uwanjani katika dakika ya 19 huku mguu wake ukiwa umepinda na nafasi yake ikachukuliwa na winga Valter Birsa
Hata hivyo mwamuzi wa pambano hilo Paolo Silvio Mazzoleni hakumpa kadi kiungo huyo wa Roma kwa kumvunja kinda huyo wa italia kwani walikuwa wakigombania mpira ambao ulikuwa nusu kwa nusu (50-50).
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0 na kuifanya AS Roma kubakia katika nafasi ya pili nyuma ya Juventus huku Chievo wakibakia nafasi ya 16 wakiwa na pointi 26 kunako ligi hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video