Nyota wa safu ya kiungo ndani ya kikosi cha City Rafael Daud atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Mgambo JKT jumapili ijayo kwenye mchezo wa ligi kuu bara kufuatia kupona majeraha aliyopata kwenye mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa Manungu mkoani Morogoro.
Akizungumza mapema leo daktari mkuu wa City Joshua Kaseko amesema Rafael alipata majeraha madogo kwenye mchezo uliopita jambo lililosababisha nyota huyo kulazimika kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Mapunda kufuatia maumivu kwenye kifundo cha mguu.
“Atakuwa ‘fiti’ kuivaa Mgambo jumapili ni matarajio yetu hasa baada ya maendeleo mazuri kufuatia matibabu ya siku hizi tatu, ni mmoja kati ya wachezaji hodari ambao wana nguvu kubwa kwenye kikosi chetu uwepo wake jumapili hii utaongeza nguvu katika kuusaka ushindi ambao ni muhimu kwetu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.
0 comments:
Post a Comment