Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kesi ya Yanga SC dhidi ya Juma Kaseja imechukua sura mpya baada ya leo Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kuagiza kesi hiyo ipelekwe katika kitengo cha uamuzi kutokana na kipa huyo kushindwa kufikia makubaliano na klabu hiyo ya Jangwani.
Machi 10 mwaka huu CMA iliwapa Yanga SC na Kaseja muda wa siku saba (Machi 10-16, 2015) kuelewana namna ya kumaliza tofauti zao, lakini imeshindikana kulisuluhisha suala hilo nje ya mahakama.
Kutokana na kutoelewana huko, Alfred Massay, msuluhishi wa CMA, ameagiza wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo jijini hapa leo kuwa kesi ipelekwe kitendo cha uamuzi cha tume hiyo.
Kaseja na wakili wake, Samson Mbamba walikuwapo wakati kesi hiyo ikinguruma kwenye tume hiyo leo huku upande wa Yanga ukiwakilishwa na Frank Chacha, Mwanasheria wa Yanga.
Katika kesi Yanga SC wanataka Kaseja awalipe zaidi ya Sh. milioni 340 zikiwa ni fidia ya kuvunja mkataba, fedha za usajili.
0 comments:
Post a Comment