Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Siku moja baada ya Stand United FC ya Shinyanga kutangaza nia ya kunasa saini ya Juma Kaseja, kipa huyo mkongwe ameibuka na kusema kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Yanga SC.
Juzi uongozi wa Stand United SC kupitia kwa mkurugenzi wake wa ufundi, Muhibu Kanu, ulisema uko mbioni kukamilisha usajili wa Kaseja ili aitumikie timu hiyo ya 'Chama la Wana' msimu ujao.
Hata hivyo, Kaseja ameuambi8a mtandao huo leo kuwa hawezi akazungumza na klabu yoyote kwa lengo la kumsajili kwa vile bado ana mkataba wa miezi tisa na Yanga SC.
"Mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga. Siwezi kuzungumza na timu nyingine kwa lengo la kunisajili kwa sababu mkataba wangu na Yanga unanibana," Kaseja amesema na kuongeza:
"Sijapewa barua ya kuachwa rasmi Yanga na mkataba wangu na Yanga unamalizika Desemba, hivyo kwa sasa kanuni zinanibana kuzungumza na klabu nyingine."
Kanuni za Usajili za FIFA zinakataza klabu kufanya mazungumzo ya kumsajili mchezaji wa klabu nyingine, ikiwa muda wa mkataba wa mchezaji husika haujabakiza chini ya miezi sita kumalizika.
Kaseja, mchezaji wa zamani wa Moro United FC, Simba SC, Yanga SC na Taifa Stars, kwa sasa ana kesi ya madai dhidi ya Yanga SC baada ya kupishana kauli na uongozi wa klabu hiyo uliotangaza kumtema.
Katika kesi hiyo inayoendelea kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Kaseja na Yanga SC jana walipewa muda na tume hiyo kukaa na kuzungumza namna ya kumalizana.
Ikiwa watashindwa kuelewana, tume hiyo ilisema jana kuwa itatoa uamuzi wa kesi hiyo kwa kuzingatia nyaraka zilizowasilishwa na pande zote mbili.
Yanga SC ndiyo waliomshtaki Kaseja katika kwenye tume hiyo wakidai fidia ya mamilioni ya shilingi kwa madai ya kuvunja mkataba kwa kukiuka masharti yaliyomo katika mkataba wa mabingwa hao mara 24 wa Tanzania Bara na kipa huyo uliosainiwa Desemba mwaka juzi.

0 comments:
Post a Comment