Tuesday, March 10, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Uongozi wa Chama la Wana, klabu ya Stand United ya Shinyanga uko mbioni kukamilisha usajili wa kipa mkongwe Juma Kaseja, imefahamika.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United FC, Muhibu Kanu, amesema Kamati ya Utendaji ya timu hiyo ya usukumani imeagiza Kaseja asajiliwe mara moja kwa ajili ya kuimarisha timu msimu ujao.

"Ni kweli tumeanza mazungumzo na Kaseja na amekubali kujiunga nasi, lakini amesema tumalizane na meneja wake. Jumatano (kesho) tutakuwa na mazungumzo na meneja na tunaamini kila kitu kitakwenda vizuri maana mchezaji ameshakubali," Kanu amesema na kuongeza:

"Kamati ya Utendaji ya Stand imeagiza usajili wetu wa msimu ujao tuanze na Kaseja. Imenikabidhi jukumu hilo nihakikishe ninamnasa Kaseja ili atuongezee nguvu. Kikao chetu na meneja wa mchezaji ndicho kitaamua atakuwa nasi kwa muda gani na kwa fungu kiasi gani."

Kaseja, mchezaji wa zamani wa Simba SC, Yanga SC na Taifa Stars, kwa sasa hana timu baada ya kutosana na Yanga SC ambao wameshamfungulia kesi ya madai mahakamani.

Hata hivyo, Kaseja amekana kufanya mazungumzo na mtu yeyote wa timu hiyo ya Chama la Wana, na hii huenda ni kukwepa kesi kwani Yanga SC bado hawajamkabidhi barua ya kumtema rasmi, hivyo anabaki kuwa mali ya wanajangwani hadi Desemba mwaka huu mkataba wake utakapofikia kikomo.

"Mimi sijazungumza na mtu yeyote kwa sasa kuhusu kunisajili. Kama yeye (Kanu) amekwambia hivyo, basi akueleze kwa kina," amesema Kaseja baada ya kutafutwa na mtandao huu jijini hapa leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video