kamati ya mashindano ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,iliyokaa kikao chake 15/03/2015 kupitoia rufaa mbalimbali kwa vilabu vinavyoshiriki ligi ya mkoa wa Dar es salaam,imetoa uamuzi wa kuitupilia mbali rufaa ya FFU FC dhidi ya SHABAB SC,wakilalamikiwa kuwachezesha wachezaji wawili kinyume na kanuni.
wachezaji hao wanaolalamikiwa ni RAMADHAN TUGA na YAKUB,walioitumikia klabu ya Shabab katika mchezo uliopigwa 10/03/2015,mchezo namba 52,na wakati huohuo wakiitumikia klabu ya Ashanti United ya Ilala katika michuano ya ligi daraja la kwanza msimu huu 2014/2015.
kamati baada ya kupitia vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa na Pan Africa,Ripoti ya mwamuzi,ripoti ya kamisaa na taarifa za usajili wa Shabab,haikuona sababu ya kubatilisha matokeo hayo ya mchezo husika ,hivyo kamati imeamua matokeo yatabaki kama yalivyotokea uwanjani kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
aidha kamati inatoa fursa kwa klabu ya Pan Africa kukata rufaa katika ngazi za juu kama hawakuridhika na uamuzi wa kamati.
WAKATI HUO HUO ,kamati imetoa uamuzi wa kuipa ushindi wa magoli 3 na pointi 3 klabu ya FFU,baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Sinza Stars wanaolalamikiwa kuwatumia wachezaji waliotumia majina yasiyokuwa yao,wachezaji hao ni Waziri Mwenzemba na Noel Ndemla,ambao majina yao kamili ni (Waziri Mwanzemba ni Tumain Agustino,na Noel Ndemla ni Mussa Hamis Ndiyunze)
wachezaji hao usajili wao upo katika vilabu vya JKT Ruvu na wakapelekwa Villa Squad kwa mkopo kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya ligi daraja la kwanza msiamu 2014/2015.
KATIKA HATUA NYINGINE,mchezo wa mtoano wa kutafuta timu itakayoungana na timu mbili zilizofanikiwa kuingia ligi ya mabingwa mkoa itapigwa 26/03/2015 katika uwanja wa Mizinga Kigamboni,ukizikutanisha timu za Pan Africa dhidi ya Changanyikeni.
mshindi katika mchezo huo ataungana na timu za Zakhem na FFC.
KASONGO AWAFAGILIA TWIGA STARS.
mwenyekiti wa DRFA Almas Kasongo,amewapongeza wachezaji wa timu ya soka ya wanawake Twiga Stars kwa mwanzo mzuri wa kuifunga timu ya taifa ya Zambia kwa mabo 4-2,katika mchezo wa marudiano uliopigwa huko Zambia.
amelipongeza pia benchi zima la ufundi la kikosia hicho kwa kazi nzuri ya kuwatengeneza vijana hao ambao wanaonesha nia ya dhati ya kutaka kusonga mbele katika mashindano hayo ya afrika.
IMETOLEWA NA DRFA
0 comments:
Post a Comment