Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kipa
Kado hakupangwa katika mechi iliyopita ambayo Coastal Union ililala kwa
bao 1-0 nyumbani dhidi ya Azam FC huku ikidaiwa kuwa amekuwa na tabia
za kuihujumu timu ya mabingwa hao wa Tanzania Bara 1988.
Baada ya kupokwa namba na kipa chipukizi Fikirini Mapala katika kikosi cha Coastal Union, kipa mzoefu Shaban Kado, ameondoka kwenye kambi ya timu hiyo bila ruhusu ya uongozi wa Wagosi hao wa Kaya huku mwenyewe akidai hana furaha ndani ya timu hiyo.
Kado amesema leo kuwa ameamua kuikacha timu hiyo kwa sababu amekuwa akipewa shutuma mbalimbali ikiwamo kuchangia timu hiyo kupata matokeo mabaya na pia kuwekwa benchi katika mechi mbili zilizochezwa kwenye uwanja wa nyumbani Mkwakwani hivi karibuni.
“Ni vigumu kufanya kazi nawatu ambao hawakuamini na wana hisia potofu kwangu nimeona ni vyema nikaondoka ili nitulize akili yangu huku nikifikiria nini cha kufanya kwa ajili ya siku zijazo," amesema Kado.
Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa Coastal Union, Akida Machai, amesema kipa huyo aliyewahi kuzidakia timu za Mtibwa Sugar FC, Yanga SC na ‘Taifa Stars’ naye alisema hakuna tatizo lolote na Kado anaruhusa maalum itakayomweka Dar es Salaam kwa wiki moja kabla ya kurejea kujiandaa na mchezo unaokuja dhidi ya Tanzania Prisons FC.

0 comments:
Post a Comment