Friday, March 20, 2015



Timu ya Juventus ya nchini italia imepata pigo kubwa baada ya kiungo tegemezi wa klabu hiyo Paul Pogba kuumia katika mechi ya juzi dhidi ya Borussia Dortmund iliyopigwa nchini Ujerumani katika dimba la Signal Iduna park.
Mfaransa huyo alitolewa katika dakika ya 27 ya mchezo huo baada ya kupata tatizo la kubanwa na misuli ya nyama za paja na nafasi yake ikachukuliwa na beki wa kati Andrea Barzagli.
Taarifa kutoka katika klabu hiyo inasema kuwa kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 50 akiuguza majeraha yake huku akiwa katika uangalizi mkali wa madaktari.
Hivyo kiungo huyo atakosa mechi za robo fainali za michuano ya klabu bingwa ulaya na ile ya marudiano dhidi ya Fiorentina kwenye kombe la Coppa Italia mwezi ujao.
Kocha wa Juventus Massimilliano Allegri anakibarua kizito kutafuta mbadala wa Pogba kwa kipindi hiki mpaka atakaporejea uwanjani mwezi April au May.
Pogba,22, amekuwa kiungo tegemezi wa wababe hao wa Italia tangu asajiliwe akiwa bado kinda mwaka 2012 akitokea kunako klabu ya Manchester United ambako alionekana hafai.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video