Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameisifu klabu ya Azam FC kuvunja ukiritimbawa Simba na Yanga katika soka ya Tanzania.
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa studio za kisasa za Azam TV, eneo la Tabata Relini, Dar es Salaam, RaisKikwete alisema mazoea ya bingwa wa Tanzania ama Simba au Yanga sasa yamevunjwa na Azam FC.
Amewasifu mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuleta changamoto mpya katika soka yaTanzania, jambo ambalo anaamini litazifanya na Simba na Yanga, vigogo vya soka nchini viamke.
Pamoja na hayo, Rais KIkwete amesifu uwekezaji wa kituo cha kisasa cha Televisheni, uliofanywa na kampuni yaBakhresa Group Limited, wamiliki wa Azam FC na Azam Media Limited, ambao waendeshaji wa Azam TV.
Rais Kikwete amesema aina ya studio aliyoishuhudia leo Azam TV ni sawa na zile za kimataifa anapokuwa katikaziara zake nchi za Ulaya na Amerika.
Pamoja na hayo, Rais Kikwete akawasihi viongozi wa Azam TV kuzingatia maadili ya taaluma ya Habari pamoja nakuweka uzalendo wa taifa lao mbele.
“Studio hii ni sawa na zile kubwa za nje, lakini ipo Tanzania na naomba ibaki kuwa ya Tanzania, mtangaze vizuri nchiyetu. Hata CNN ni ya Marekani, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Marekani, inabaki kuwa yaMarekani,”.
“Hata BBC, ni ya Uingereza, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Uingereza, inabaki kuwa yaUingereza. Hata Aljazeera ni ya Qatar, inatangaza mambo ya nje, lakini linapokuja suala la Qatar, inabaki kuwa hyaQatar. Kwa hiyo na nyinyi, naomba TV yenu ibaki kuwa ya Tanzania,”alisema Rais Kikwete.
Rais huyo anayemaliza muda wake Oktoba mwaka huu, amesema kwamba amefurahishwa na uwekezaji huomkubwa, wenye hadhi na thamani, ambao utatoa ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresaamesema kwamba kwa kipindi cha miongo minne sasa tangu wameanza shughuli za kuwahudumia Watanzaniakatika nyanja tofauti- ubora, upatikanaji wa uhakika na gaharama nafuu umekuwa muongozo wao katika biasharazao.
“Nyote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumeendelea kuwahudumia Watanzania na kwa namna ya kipekee, Mh.Rais tunawashukuru sana Watanzania kwa kuendelea kutuunga mkono na tunawaomba waendelee kutuungamkono, kwa hakika ubora na unafuu kwetu ni silaha na jambo muhimu tunalolizingatia katika hudumazetu,”amesema.
Alhaj Bakhresa amesema kwamba, hivi karibuni Makampuni yao yalijinyakulia nafasi za juu katika ubora wa viwango,na kwamba dhamira hiyo wanaielekeza pia katika huduma yao mpya ya matangazo ya Televisheni, ili kuendeleakuunga mkono sera za Taifa na mpango wa kusambaza taarifa sahihi na za haraka kwa Watanzania.
Awali ya hapo, Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando alisema kwamba katika kipindi hiki kifupi,Azam Media Group imefanikiwa kupata ufanisi wa kuridhisha mno hata kuweza kujijengea heshima na kufahamikavyema hasa katika utangazaji wa michezo na hususan soka.
“Pamoja na kuanzishwa kwa timu ya kandanda ya Azam, ambayo nayo kwa kipindi kifupi sana imeweza kupaa hadikunyakua ubingwa wa kandanda wa nchi hii, hivi sasa ndiyo klabu bingwa ya kandanda Tanzania, uongozi wa SSBukaonea uimarishe ari hiyo ya kuendeleza michezo nchini kwa kwenda hatua moja zaidi mbele na ndipo ikazaliwaAzam Media Limited ,” amesema Mhando.
Amesema ushirikiano uliofikiwa haraka baina ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umefanikishakwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii kuonyeshwa moja kwa moja kwa mechi za Ligi Kuu ya taifa nakuifanya ligi hiyo hivi sasa iimarike sana na kuwa ya kusisimua zaidi.
“Kama ilivyo Ligi Kuu ya England, hivi sasa ligi yetu hii imefikia mahala ambapo haitabiriki. Mfano Mheshimiwa Raisni hapa majuzi tu ambapo bila ya shaka vijana wapya wa Stand United ya Shinyanga walikufurahisha tena live kwakuwachakaza watani wako Simba,”alisema huku akicheka akimtazama Rais Kikwete ambaye ni mpenzi wa YangaSC.
Mhando amesema mafanikio hayo ni makubwa ambayo ukichanganya na juhudi za Rais Kikwete kwenye michezo,Watanzania watarajie kwa kipindi kifupi kijacho wataanza kuvuna matokeo ya kufurahisha kwenye michezo.
“Na kwa kuwa wewe, Mheshimiwa Rais, vile vile ni mshabiki na mpenzi mkubwa wa mchezo wa kikapu, bila ya shakasiku hizi unapopata wasaa hukosi kuangalia “live” zikionyeshwa na Azam TV, kila ijumaa usiku, mechi za michuanoya ligi ya mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam,”.
“Naambiwa kutokana na hatua hii, ule ushindani uliokuwepo zamani ya klabu za Pazi na Tan Blacks umeanza tenakwa kasi kubwa na hivyo kuufanya mchezo wa kikapu kupata maendeleo ya haraka sana,”ameongeza Tido.
Amesema uwekezaji huo wenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 500 umefanywa kwa mpangilio wakiwango cha juu na wawekezaji wazalendo kwa nia na ari kama ile ile, ya kuifanya Azam TV kuwa BBC ya Tanzania, CNN ya Afrika Mashariki na Al Jazeera ya Afrika,”.
“Tunafahamu ya kwamba wewe ni muumini wa kila jambo kufanywa kwa weledi na ubunifu wa kiwango cha juuTunakuahidi ya kwamba katika muda siyo mrefu utaweza kuuona weledi huo na kushuhudia ubunifu wa kiwango chajuu sana hapa hapa Azam TV,”.
“Tumejipanga vizuri na tuna mipango mikubwa sana ya kufika kileleni na kuwa Televisheni namba moja nchini hapakatika kipindi kifupi sana kijacho kwani kama ulivyoona tunavyo na kutumia vifaa bora na vya kisasa kabisa vyautangazaji na kuwa hivi sasa tunaimarisha mno idara yetu ya rasilimali watu kwani tunaelewa ya kwamba bila ya waohatutaweza kutimiza ndoto yetu hii kubwa,”alisema kumuambia Rais Kikwete.
Viongozi mbalimbali wa dini, siasa na taasisi mbalimbali zikiwemo za vyombo vya Habari pamoja na wasanii nyotawalihudhuria zoezi hilo lililofana, likichombezwa na burudani za wasanii wa nyumbani.
0 comments:
Post a Comment