MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Radamel Falcao bado ana imani kuwa ataendelea kubakia Old Trafford msimu ujao.
Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amefunga magoli manne tu katika mechi 19 alizocheza kwenye kikosi cha Louis van Gaal msimu huu na anatarajia kureja tena Monaco kabla ya kufirikia kwenda kwa mkopo mwingine katika klabu za Juventus, Valencia au Real Madrid.
Falcao mwenye miaka 29 alikuwa katika kiwango cha juu akilichezea taifa lake siku tano zilizopita ambapo alifunga magoli matatu katika mechi mbili dhidi ya Bahrain na Kuwait na kufikia rekodi ya ufungaji wa magoli mengi kwa wakati wote akifikisha mabao 24.
'Nadhani ninapofunga siku zote ni muhimu sana na inanifanya nijiamini. Nilicheza kwa kiwango changu cha juu na kufunga, sasa narudi Manchester nikijiamini zaidi"
0 comments:
Post a Comment