Baada ya kufanikiwa kuipatia Simba Pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzana bara, kwa kuifungia timu yake Simba SC, Mshambuliaji wa klabu hiyo Emannuel Okwi amesema kuwa goli hilo analipeleka kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha sikukuu yao leo.
Okwi akiongea
Baada ya mchezo huo kumalizika, Okwi alisema kuwa anawapenda sana wanawake wote hivyo bao hilo alilofunga liwe ni zawadi yao.
"kucheza kwa kujituma, umakini na kujiamini ndio kumetupa Ushindi, Goli nawapa wanawake wote, leo (jana) ni siku yao ninawapenda wote” Amesema Okwi.
Kufuatia ushindi huo Simba SC, inakuwa imepaa hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 26 huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili kwa alama 30 nyuma ya Yanga SC wenye pointi 31.
0 comments:
Post a Comment