TIMU ya Coastal Union imewasilia jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha wapinzani wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi ijayo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa sasa nguvu zao watazielekeza kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye mjini hapa.
Amesema kuwa dhamira yake aliyoipanga ni kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting haikuweza kutimia na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 hivyo atahakikisha inatimia kwenye mechi hiyo.
Amesema timu hiyo imerudi salama mkoani hapa na tayari wameshaanza kujipanga imara kuhakikisha mechi hiyo timu inapata ushindi n kutokana na uimara wa kikosi chao
Aidha amesema kuwa wachezaji wa kikosi hicho wameimarika zaidi na wapo imara kuweza kupambana kufa na kupona ili kuchukua pointi tatu muhimuzo zitawasogeza kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Hata hiyo amewataka wapenzi na mashabiki wa soka mkoani hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuipa hamasa timu hiyo kuweza kutimiza ndoto zake.
0 comments:
Post a Comment