Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema iwapo kikosi chake kitaendelea na kasi
walionayo kwa sasa basi watafanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu soka nchini uingereza msimu huu.
Rodgers aliyasema hayo baada ya Liverpool kupata ushindi wake wa tano mfululizo ilipoilaza Swansea 1-0 jumatatu usiku na kupata pointi tatu muhimu katika mtanange huo.
Bao la pekee katika mechi hiyo ilipachikwa kimiani na Jordan Henderson, Liverpool
inashikilia nafasi ya 5 hivi sasa katika jedwali la msimamo wa ligi kuu ya
Uingereza wakiwa wamesalia na mechi 9 za kuchezwa msimu huu.
Majogoo hao wamejizolea alama 54 alama nne tu nyuma ya mabingwa watetezi Manchester City ambao waliambulia kichapo cha bao moja kwa nunge kutoka kwa Burnley mwishoni mwa wiki iliyopita.
"Baada
ya matokeo ya Manchester City dhidi ya Burnley ninahakika tuko katika
nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya pili,Motisha wetu hivi sasa uko juu na hivyo itatusaidia kukabili mechi zetu zote zilizosalia."alisema Rodgers.
0 comments:
Post a Comment