Ile safari ndefu ya Brazil kufuta huzuni na fedheha kubwa waliyopata
Nyumbani kwao Sao Paulo Mwaka Jana walipobamizwa 7-1 na Germany kwenye hatua ya
Nusu Fainali ya Kombe la Dunia, ilipungua Juzi huko Paris walipoitwanga
France 3-1mabao ya naodha Neymar,Oscar na Luis Gustavo, lakini kesho Jumapili wapo London Uwanja wa Emirates kucheza na Chile
katika Mechi nyingine ya Kirafiki.
Tangu fedheha ya Sao Paulo, Brazil wakiwa chini ya Kocha mpya Dunga na Kepteni mpya Neymar wameshinda Mechi zao zote 7.
Jumapili wataivaa Chile, ambao ni wenzao kutoka Marekani ya Kusini,
watakaoongozwa na Alexis Sanchez ambae Emirates ni Uwanja wa Nyumbani
kwa vile Klabu yake ni Arsenal.
Mbali na Neymar, Brazil ya Dunga inang'ara kutokana na umahiri wa
Wachezaji wake hasa David Luiz, Oscar na Roberto Firminho.
Mechi na Chile ni moja ya matayarisho ya Brazil kwa ajili ya kombe la Copa
America, Mashindano ya Nchi za Marekani ya Kusini, yatakayochezwa huko
Chile kuanzia Mwezi Juni mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment