Wakati huo timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni
(Beach Soccer) inarejea leo mchana saa 8:45, kwa Shirika la Ndege la Ethiopia
ikitokea nchini Misri ambapo jana ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa
kufungwa 9-4 na wenyeji.
Rais Malinzi amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata
matokeo mazuri katika mchezo wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu
ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki
michuano hiyo ikiwa ni miezi sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini
Tanzania.
Ili kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo
huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha
mpira wa ufukweni katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa
ambapo mchezo huo unachezwa Dar es salaam na Zanzibar.
Katika mchezo wa jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally
Rabbi (3) Kashiru Salum (1), Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za
Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la
Ufukweni Visiwa vya Shelisheli, zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara
ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.
0 comments:
Post a Comment