Monday, March 30, 2015



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, kiungo  Abdi Hassan Banda amemtandika ngumi kiungo mshambuliaji Ibrahim Hajibu katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika jioni ya leo uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mwandishi wa MPENJA BLOG, ameshuhudia Hajibu akimkwatua Banda kwa nyuma tukio ambalo Banda alichukulia kawaida, dakika chache baadaye Hajibu akamrukia na kumpiga teke begani, ndipo Banda alipocharuka na kuanza kurushiana maneno.
Hajibu alimjibu vibaya Banda na ndipo nyota huyo wa zamani wa Coastal Union alimpiga ngumi kali iliyomkera Hajibu na kutaka kujibu mapigo.
Wachezaji walimshika Hajibu kabla ya kutimiza nia yake na Ramadhan Singano akamuondoa Banda eneo la tukio.
Baada ya tukio hilo, kocha mkuu, Goran Kopunovic aliwaita Hajibu na Banda na kuwapa nasaha akiwasihi waache mambo ya kitoto na warudi uwanjani.
Nyota hao wawili waliingia mchezoni na kusahau tofauti zao.
Hata hivyo, Kiongozi mmoja wa Simba amekiri kuwa Banda huwa ana maamuzi ya haraka ya kupigana anapofanyiwa vibaya, lakini Hajibu naye ana maneno ya 'shombo'. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video