YANGA wameishusha Azam fc kileleni mwa ligi kuu soka Tanzania bara kufuatia kushinda mabao 2-1 jioni ya leo dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Taifa wa Dar es salaam.
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na Saimon Msuva dakika ya nane kwa mkwaju wa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Benjamini Asukile.
Naye Amissi Tambwe alifunga bao la pili dakika ya 15 akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa
Bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Salum Kanoni kwa penalti baada ya beki Rajab Zahir kumuangusha eneo la hatari Atupele Green.
Kwa matokeo hayo, Yanga wamefikisha pointi 41 kileleni, pointi moja zaidi ya Azam fc walioshuka nafasi ya pili.
Yanga wameshinda mabao mengi, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini.
Pia walicheza kwa mbwembwe baada ya kufunga magoli mawili ya mapema na waliwaruhusu Kagera watulie.
Baada ya ushindi wa leo, Yanga wanashuka dimbani jumamosi kuikabili Mgambo JKT "Wazee wa Mguu pande' katika uwanja mgumu wa vigogo wa soka nchinhi, CCM Mkwakwani Tanga.
msimu uliopita, Yanga walifungwa 2-1 na Mgambo Mkwakwani na kwa kiasi kikubwa kipigo hicho kilifuta ndoto za ubingwa ambao ulitwaaliwa na Azam fc.
Nao Azam fc watashunda uwanjani Mkwakwani jumapili kuwakabili wenyeji Coastal Union.
0 comments:
Post a Comment