Tuesday, March 10, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Baada ya kusimamishwa na uongozi wa Mbeya City,golikipa David Burhan amekaribisha ofa za kujiunga na timu nyingine ili achane na kikosi cha mbeya City FC.

Burhan, kipa wa zamani wa Tanzania Prisons FC na kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/13, alisimamishwa na Bodi ya Michezo ya Jiji la Mbeya kuidakia Mbeya City FC kwa madai ya kufungwa bao la kizembe na winga Mrisho Ngasa wa Yanga SC katika mechi yao iliyopita jijini Mbeya.


Mbeya City FC inayonolewa na Kocha Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Juma Mwambusi, ililala kwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya wiki mbili zilizopita.

Ngasa alifunga bao lisilotarajiwa katika dakika ya 59 alipounasa mpira uliokuwa miguuni mwa kipa Burhani aliyetaka kumpiga chenga winga huyo wa zamani wa Kagera Sugar FC, Azam FC na Simba SC.

Katika mahojiano na mtandao huu leo jioni, Burhan amesema yuko tayari kujiunga na timu yoyote itakayompa ofa nzuri.

"Kwa sasa mimi bado ni mchezaji wa Mbeya City FC licha ya kusimamishwa. Stahiki zangu zote ninapata. Kwa kuwa mkataba wangu na klabu hii umebaki miezi mitatu, ninaruhusiwa kuzungumza na klabu nyingine kwa nia ya kunisajili," amesema Burhan.

Kanuni za Usajili ya FIFA zinampa idhini mchezaji kuzungumza na timu nyingine kuhusu kumsajili kama mkataba wa mchezaji husika umebakiza muda ambao si zaidi ya miezi sita.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video